Balozi Kasike awatafutia Watanzania fursa Eswatini

MBABANE-Mheshimiwa Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji ambaye pia anawakilisha Ufalme wa Eswatini na Jamhuri ya Madagascar, amekutana na Mhe. Jane Matty Mkhonta-Simelane, Waziri wa Utalii na Mazingira wa Ufalme wa Eswatini jijini Mbabane.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Machi 27,2024 na Ubalozi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Maputo, Msumbiji.

Mkutano huo ulifanyika wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Balozi Kasike Ufalme wa Eswatini ambako anakutana na viongozi wa Serikali na taasisi mbalimbali zinazoshughulika na Masuala ya Uchumi, Biashara na Uwekezaji kwa ajili ya kutangaza fursa na kutafuta masoko ya bidhaa za Tanzania.
Pamoja na masuala mengine, Viongozi hao wawili walikubaliana kuanzisha na kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Eswatini katika Sekta ya Utalii hasa kutokana na vivutio mbalimbali vilivyopo kwenye nchi hizi mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news