Fomu ya Urais ni moja-Waziri Mkuu

DAR ES SALAAM-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameongoza uchangishaji wa fedha shilingi milioni 120 kwa ajili ya kumuwezesha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuchukua fomu ya kugombea Urais mwaka 2025.
Fedha hizo zimechangwa wakati wa mkutano wa Wanawake wa kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa Kinara wa Nishati Safi ya kupikia, Mazingira na Afya ya Mama na Mtoto.

Fedha hizo zimekabidhiwa kwa Waziri Mkuu na Waziri wa maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum Mhe. Doroth Gwajima kwa niaba ya wanawake hao.

Ameyasema hayo leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam ambako ni mgeni rasmi katika Mkutano wa Wanawake wa Kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa Kinara wa Nishati Safi ya kupikia, Mazingira na Afya ya Mama na Mtoto.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news