Prof.Muhongo agawa maarifa jimboni

MARA-Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara,Prof. Sospeter Muhongo anaendelea kugawa vitabu viwili vinavyoelezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2020-2025 ndani ya jimbo hilo.
Viongozi wa CCM na wananchi wa Kata ya Suguti wakiwa wamebeba nakala za vitabu vilivyotolewa jimboni humo.
Mbunge Prof. Muhongo akiipatia Kata ya Suguti simu mpya ya kuandikishia wanachama wa CCM.

Hatua hiyo inalenga kila mmoja aweze kuyaona yaliyotekelezwa jimboni humo na kisha kuandikwa kwenye vitabu hivyo, ambapo vimekuwa vikitolewa bure.
Wanafunzi wa Suguti Sekondari wakisikiliza mafunzo ya utunzaji wa misitu yaliyotolewa na Meneja wa Misitu (TFS) Wilaya ya Musoma,Boniphace Kareberege.

"Vitabu hivi vya rangi vinagawiwa bure kwa viongozi wa chama (CCM) wa ngazi zote na wananchi wengine ndani wa Jimbo la Musoma Vijijini. Viongozi wa Serikali nao wanagawiwa vitabu hivi,"imeeleza taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo hilo Machi 22, 2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news