Rotary Club ya Zanzibar yasisitiza umuhimu wa kuchunguza afya

ZANZIBAR-Rais wa Rotary Club ya Zanzibar Stone Town,Augustine Mwombeki ameishauri jamii kuwa na tabia ya kuchunguza afya mara kwa mara ili kugundua magonjwa nyemelezi na kupata tiba mapema.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kambi ya uchunguzi na matibabu bure kwa wananchi wa Makunduchi iliyofanyika Skuli ya Kiongoni Mkoa wa Kusini Unguja amesema, endapo jamii itaendeleza utamaduni huo itasaidia kugundua maradhi katika hatua za awali na kupatiwa matibabu kwa muda stahiki.

Amesema, uwepo wa kambi za uchunguzi na matibu vijijini kunahamsisha na kushajihisha wananchi kujitokeza kuchunguza afya zao na kuishauri jamii kuchangamkia fursa za kambi hizo pale zinapotokezea.

Aidha, alizitaka taasisi nyingine za Serikali na binafsi kushirikiana kujidhatiti kutoa huduma bora za afya kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuunga mkono kambi kama hizo ziweze kufanyika mara kwa mara vijijini, kwani wamekuwa wazito kwenda hospitali na kuishia kutumia mitishamba jambo ambalo linahatarisha afya zao.

Amefafanua kuwa, kambi hiyo ni kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa maradhi mbalimbali kwa watoto, wazee na kina mama wapatao 1,500 ambapo wamejipanga kutoa huduma tofauti zikiwemo uchunguzi wa magonjwa ya meno,macho,ngozi,masikio, koo na pua, HIV pamoja na magonjwa ya kina mama katika kijiji hicho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news