Simba SC yapoteza nyumbani dhidi ya Al Ahly

DAR ES SALAAM-Mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Simba SC dhidi ya Al Ahly uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa umemalizika kwa kupoteza kwa bao moja.
Machi 29,2024 Al Ahly walipata bao mapema dakika ya nne kupitia kwa Ahmed Kouka.

Ni baada ya mpira wa krosi uliopigwa na Mohamed Hany kushindwa kuzuiliwa vizuri na mlinzi Henock Inonga kabla ya kumkuta mfungaji.

Baada ya bao hilo Al Ahly walirudi nyuma wakizuia na kuwaacha, Simba SC wamiliki mpira huku wao wakifanya mashambulizi machache ya kushtukiza.

Hata hivyo, Simba SC walistahili kwenda mapumziko tukiwa mbele kwa zaidi ya mabao mawili baada ya kupoteza nafasi mbili za wazi kupitia kwa Sadio Kanoute na Saido Ntibazonkiza.

Kipindi cha pili walirudi kwa kasi na kuendelea kuliandama lango la Al Ahly,lakini walikosa umakini wa kutumia nafasi walizotengeza.

Mchezo wa marudiano utapigwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Cairo nchini Misri Aprili 5,mwaka huu na mshindi wa jumla atasonga mbele na kutinga nusu fainali kupitia michuano hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news