TanTrade yakutana na TASSIM

DAR ES SALAAM-Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bi. Latifa Khamis, amekutana na Mtendaji Mkuu wa Tanzania Association of Small Scale Industries and Manufactures (TASSIM), Bw. Elia Joseph ambaye ametembelea ofisi za TanTrade na ujumbe wake.

Lengo likiwa ni kuitambulisha TASSIM na kueleza shughuli wanazozifanya katika kuendeleza viwanda Vidogo ili kukua katika soko kubwa lenye ushindani.
Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade amewapongeza TASSIM na kushauri washiriki shughuli zote za ukuzaji Biashara za TanTrade ndani na Nje ya Nchi ambapo huwa na lengo la kuendeleza na kutafuta masoko ya bidhaa za Tanzania ili kuwezesha Viwanda hivyo kupata wateja. 

Aidha,alisistiza Taasisi ya TASSIM kushiriki Maonesho ya 48 Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayotarajiwa kuanza tarehe 28 Juni hadi tarehe 13 Julai 2024 pamoja na maonesho ya TIMEXPO ambayo huandaliwa na TanTrade kwa kushirikiana na CTI kutangaza Bidhaa za Viwanda nchini.

Kwa upande mwingine Mtendaji Mkuu wa TASSIM amemshukuru Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade kwa mapokezi mazuri na kuahidi ushirikiano zaidi pia kwa kuhusisha Taasisi zingine za wazalishaji ili kufikia malengo ya kuinua viwanda vidogo nchini (SMEs) ambao ni wengi lakini bado hawajaweza kuwa kwenye kundi kama ilivyo kwa wazalishaji wakubwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news