Vijibweni waadhimisha miaka mitatu ya Rais Dkt.Samia kwa kufurahia anuani za makazi

NA JAMES K.MWANAMYOTO

TUKIWA tunaendelea kuadhimisha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, wananchi wa Kata ya Vijibweni Kigamboni wamefurahishwa na kitendo cha Serikali ya Awamu ya Sita kutekeleza mpango wa Anuani za Makazi kwa kuwezesha upatikanaji wa barua ya utambulisho kwa njia ya kielektroni kupitia App(napa), Tovuti (napa.mawasiliano.go.tz) na USSD (viswaswadu *152*00#).
Mhandisi wa Mifumo wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia Bw. Medson Naftali akizungumza na Mkazi wa Mtaa wa Mnyamani Vijibweni Kigamboni, Mzee Omary Mnyamani aliyejitolea sehemu ya kiwanja chake kwa ajili ya barabara ya Mnyamani iliyopewa jina la mzee huyo.
Mtendaji wa Mtaa wa Kibene Kata ya Vijibweni Kigamboni, Bw. Banyanga Juma akionesha kibao cha Mtaa wa Barabara ya Mnyamani kwa Mhandisi wa Mifumo kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia, Bw.Medson Naftali.

Mtendaji wa Mtaa wa Kibene Kata ya Vijibweni, Bw. Banyanga Juma amesema, upatikanaji wa barua kwa njia ya kielektroniki unamuondolea mwananchi usumbufu wa kulazimika kwenda kwa mjumbe na kwenye Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa, inamuwezesha yeye binafsi kutoa huduma hiyo ya barua kwa wakati na kuongeza kuwa, anuani za makazi zinamuwezesha kutambua kirahisi makazi ya wananchi anaowaongoza.

Naye, Mkazi wa Mtaa wa Mnyamani, Mzee Omary Mnyamani amesema, uwepo wa anuani za makazi unawawezesha ndugu, jamaa na marafiki zake kufika kirahisi nyumbani kwake kwani nyumba yake ina utambulisho wa namba 8 hivyo ni rahisi kwa kila anaemuhitaji kufika nyumbani kwake.
Mkazi wa Mtaa wa Mnyamani Vijibweni Kigamboni, Mzee Omary Mnyamani akieleza faida za uwepo wa anuani ya makazi katika eneo analoishi.
Mkazi wa Mtaa wa Mnyamani Vijibweni Kigamboni, Mzee Omary Mnyamani akipongezwa na Afisa Hesabu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia Bw. Shakibu Nsekela kwa kutoa eneo lake kwa ajili ya barabara katika Mtaa wa Mnyamani uliopewa jina lake ikiwa ni sehemu ya kuenzi mchango wake.

Aidha, Mhandisi wa Mifumo wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia Bw. Medson Naftali amefurahishwa namna mtaa wa Mnyamani ulivyopangiliwa na amempongeza Mzee Omary Mnyamani kwa kutoa sehemu ya eneo lake kwa ajili ya barabara katika Mtaa wa Mnyamani uliopo kata ya Vijibweni Kigamboni.

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia na Ofisi ya Rais-TAMISEMI zinashirikiana kiutendaji katika kuwezesha upatikanaji wa anuani za makazi nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news