Wanawake NHC wasafiri kilomita 900 kutoa tabasamu kwa watoto yatima

KATAVI-Wanawake watumishi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wamesafiri zaidi ya kilomita 900 kutoka jijini Dar es Salaam hadi mkoani Katavi kwa ajili ya kuwapatia misaada watoto wenye mahitaji maalum.
Safari hiyo ambayo imekuwa ya faraja kwa watoto wa Kituo cha Watoto Yatima Nsemulwa cha Masista wa Maria Mtakatifu Malkia wa Afrika Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda ilikuwa ni katika shamrashamra za kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani.
Hatua hiyo ni utekelezaji wa Sera ya Huduma kwa Jamii (CSR) ya shirika hilo ambayo lengo lake ni kuhudumia jamii katika nyanja ya elimu, afya na makundi maalum nchini.

Wakiwa kituoni hapo, wawakilishi wa NHC leo Machi 8, 2024 wamepokea hati ya shukrani kutoka kwa Kituo cha Watoto Yatima Nsemulwa cha Masista wa Maria Mtakatifu Malkia wa Afrika Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda.

Hati hiyo ya shukrani imekabidhiwa kwa NHC na Mratibu wa Kituo hicho, Sista Rose Sungura, kufuatia msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa kwa ajili ya watoto hao.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Sista Sungura amesema, vitu walivyopokea vimekuja kwa wakati muafaka kutokana na uhitaji wake kwa sasa.
Amesema, NHC imeonesha thamani kubwa ya malezi kupitia vitu vilivyotolewa, kwani vitasaidia katika kukidhi mahitaji ya watoto kituoni hapo.

"Hatuna cha kuwalipa Mungu awalipe sawasawa na mapenzi yake, kitendo cha kutoka Dar es Salaam kuja hadi Katavi kwa ajili ya yatima.
"Huu ni uungwana mkubwa sana mliouonesha kwani mmeacha vituo vingapi uko hadi mkaamua kutufikia sisi tena tuliopo pembezoni huku kwa kweli Mungu awabariki sana katika kazi zenu, na Mkurugenzi Mkuu uliyeruhusu haya yafanyike baraka za Mungu zikushukie katika utendaji kazi wako," amesema Sista Sungura.
Akikabidhi msaada huo Afisa Habari wa NHC, Bi. Domina Rwemanyila amesema kuwa, msaada huo umetolewa mahsusi kwa watoto hao ikiwa ni kujali watoto walio katika mazingira magumu kwa kuwaonesha thamani yao duniani.
Rwemanyika amesema,pia huo ni mchango wa wanawake wa NHC katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8 kila mwaka.
Baadhi ya vitu vilivyotolewa ni sabuni za kufulia, kuogea, maziwa ya kopo, mabegi ya shule, penseli, sukari, sembe, mafuta ya kupikia, kanga, pampers, mafuta ya kujipaka na unga wa ngano.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news