Waziri Mkuu atoa maagizo kwa halmashauri nchini

LINDI-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezielekeza Halmashauri zote zinazotekeleza mradi wa Mpango wa Matumizi ya Ardhi ya Vijiji kuandaa mpango wa ufuatiliaji na tathmini ili kupima ufanisi wa utekelezaji wa mradi huo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia wakati wa Mkutano wadau kujadili utekelezaji Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Rangwa Pride mkoani Lindi tarehe 22 Machi, 2024. Mkutano huo umebebwa na kaulimbiu isemayo; “Usawa wa Kijinsia katika Umiliki wa Ardhi kwa Ustawi wa Jamii”. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Ametoa maelekezo hayo leo Ijumaa, Machi 22, 2024 wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa Kujadili Utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi uliofanyika wilayani Ruangwa mkoani Lindi.

Waziri Mkuu pia amezielekeza Halmashauri zote ziandae mpango mahsusi wa kupata suhulu ya migogoro inayohusu mipaka ya vijiji. “Lengo la Serikali ni kupima ardhi yote nchini ili wananchi wakiwepo wanavijiji waweze kuitumia katika kufanya shughuli za kiuchumi, Wenyeviti wa Halmshauri hakikisheni mnatoa ushirikiano kwa Timu inayotekeleza mradi ili mapungufu yaliyopo yapatiwe suluhu”.
“Nisisitize Wakuu wa Wilaya, Wakurugnzi wa Halmashauri, Wenyeviti na Watendaji katika vijiji washiriki kikamilifu kuwafikia wananchi na kuwaelimisha umuhimu wa matumizi sahihi ya ardhi, ili waweze kunufaika pamoja na kupata hati miliki za ardhi wanayoimiliki” ameeleza Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu pia amewataka Watalaam wa sekta ya ardhi, kushirikiana na viongozi wa Serikali za mitaa na vijiji katika hatua zote za utekelezaji wa mradi.
Amesema kuwaelimisha viongozi hao kutawasaidia katika kuhamasisha wananchi, lakini pia kutoa elimu kuhusu masuala ya ardhi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda, amesema mradi huo unategemea kutekelezwa katika Halmashauri za Wilaya zilizoko kwenye mpaka wa kimataifa wa nchi, Wilaya zenye migogoro mingi ya matumizi ya ardhi na Wilaya zenye fursa kubwa za kiuchumi.

Amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazokabiliwa na kasi kubwa ya ukuaji wa miji na vijiji kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu linalosababisha kuongezeka kwa mahitaji ya ardhi iliyopangwa na yenye usimamizi mzuri na salama, hivyo uboreshaji wa milki za ardhi utaenda kuwa suluhu.

Kwa upande wake Meneja wa Mradi Vijijini Joseph Osena, amesema kuwa Mradi huo wa Uboreshaji usalama wa milki za Ardhi unaenda kutatua changamoto nyingi za ardhi ambazo zimekuwa zikiyakumba maeneo mengi nchini.
Amewataka viongozi wa kijamii kutoa ushirikiano kwa timu ya watekelezaji wa mradi huo, ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa zoezi hilo.

Naye Diwani wa Kata ya Ruangwa Halima Mponda, ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maeneo ya Makazi kwa juhudi inazozifanya katika kupima vijiji hali ambayo inaenda kumaliza migogoro mingi iliyokuwa inatokea.

Mradi wa uborshaji wa usalama wa miliki za Adhi (LTIP) unasimamiwa na Wizara ya Adhi Nyumba na Mandeleo ya Makazi ukiwa na kauli mbiu isemayo; “Usawa wa Kijinsia katika Umiliki wa Ardhi katika ustawi wa Jamii”.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news