Mhadhiri ashtakiwa kwa kuomba rushwa ya ngono

TABORA-Aprili 25, 2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Tabora, mbele ya Mhe. Demetrio Nyakunga, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Tabora, imefunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi Namba ECC. 10892/ 2024 ya Jamhuri dhidi ya Bw. Michael Fredrick Mgongo ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Cha Utumishi wa Umma (TPSC) Tawi la Tabora.

Mwendesha Mashtaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Bi. Mwanaidi Mbuguni ameieleza Mahakama kwamba,mshtakiwa aliomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma (Uhazili) ili amfanyie upendeleo na kumfaulisha masomo aliyofeli.

Mshtakiwa alisomewa mashtaka yanayomkabili na kukana mashtaka hayo.

Aidha,mshtakiwa alikidhi masharti ya dhamana na yuko nje kwa dhamana ambapo kesi hiyo itakuja tena Mei 23,2024 kwa ajili ya kusoma hoja za awali kwa mshtakiwa na kuanza kusikilizwa kwa upande wa Jamhuri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news