Mheshimiwa Chumi ampongeza Rais Dkt.Samia kwa kuipa nishati safi na salama kipaumbele nchini

IRINGA-Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini, Cosato Chumi ameipongeza Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha jitihada za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya salama kwa jamii.
Akizungumza wakati wa mafunzo kuhusu matumizi ya nishafi safi na salama aliyoandaa kwa makundi mbalimbali, Chumi ameeleza umuhimu wa kuelekeza juhudi kwenye matumizi ya nishati rafiki kwa mazingira.

Katika mafunzo hayo ambayo yametolewa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), yamehudhuriwa na viongozi wa dini, viongozi wa chama, viongozi wa serikali za mitaa na vijiji na wazee maarufu, jumla ya mitungi ya gesi 350 iligawiwa kwa washiriki wa mafunzo hayo ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi na salama kwa wananchi.

Mbunge Chumi amesema, lengo la mafunzo hayo ni kuwapa viongozi hao elimu ili waweze kuwa mabalozi wa kuelimisjha kuhusu matumizi ya nishati safi na salama, na kwa kufanya hivyo kutasaidia kulinda mazingira kwa kutumia nishati safi na salama.

Chumi amesema, mafunzo hayo yatasaidia kutoa elimu kuhusu maana ya nishati safi na salama kutoka kwa wataalamu, pamoja na athari za matumizi ya nishati zisizo salama na mpango huo wa kugawa mitungi ya gesi unalenga kuhamasisha wananchi kutumia nishati safi kwa gharama nafuu kwani hata ujazo wa mitungi hiyo ni mdogo utakao saidia wananchi wengi kumudu kununua licha ya hali tofauti za wananchi.

"Kupitia jitihada hizi tunatarajia jamii itapunguza matumizi ya nishati ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa katika uharibifu wa mazingira huku ikidumisha ustawi na maendeleo ya jamii."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news