Mvua, upepo mkali yasababisha maafa Musoma

NA FRESHA KINASA

MVUA kubwa iliyonyesha Aprili 5,2024 huku ikiambatana na upepo mkali imesababisha maafa makubwa katika Kijiji cha Lyasembe Kata ya Murangi Wilaya ya Musoma, ambapo imeathiri watu 685 kati yao watoto ni 384 na watu wazima 301.
Hayo yamebainishwa Aprili 8, 2024 kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, nyumba zilizobomoka ni 17 za wanakijiji,nyumba zilizoezuliwa mapaa ni 61 ambapo nyumba 59 ni za wanakijiji na vyumba viwili vya madarasa ya Shule ya Msingi Lyasembe. Huku miti ya shule iliyoharibiwa na upepo mkali ikiwa ni 40.
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo akiwa shuleni Lyasembe kushuhudia uharibifu mkubwa uliobabishwa na mvua kubwa na upepo mkali.

Miti mikubwa iliyong'olewa mizizi ni 28,miti iliyovunjiwa matawi makubwa ni 12.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Serikali ya kijiji inaomba misaada ya aina mbalimbali hususani vifaa vya ujenzi ikiwa ni pamoja na saruji, mabati, mbao na misumari.

Huku taarifa hiyo pia ikielekeza kuwa fedha za michango zipelekwe kwenye Akaunti ya Kijiji ambayo ni BMB akaunti Na: 30302300012 ambayo ni ya Kijiji cha Lyasembe.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma (DC), Dkt Khalfany Haule na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, na wananchi waathirika wakiwa kwenye eneo la maafa Kijijini Lyasembe.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Shule ya Msingi Lyasembe ilifunguliwa mwaka 1975, kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 811, na walimu 10.

Na ina jumla ya vyumba vya madarasa 10, kati ya hayo matano ni chakavu. Mawili kati ya hayo chakavu yameezuliwa mapaa. Na Mahitaji halisi ya shule hiyo ni vyumba vya madarasa 21, na nyumba za walimu 10 (two in one).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news