Wasomewa mashtaka 18 Ilala, kikundi hewa chanzo

DAR ES SALAAM-Washitakiwa wanne katika Halmashauri ya Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam wamesomewa jumla ya mashtaka 18 ya Kughushi, Uhujumu Uchumi na Utakatishaji Fedha Haramu.
Washitakiwa hao ni Sefania Adam Mwanja ambaye ni Mweka Hazina wa Kikundi cha Afya Jamii,Eric Isack Gabriel ambaye ni Mtaalamu wa Maabara.

Wengine ni Sabina William Ndasi ambaye ni Mtendaji wa Mtaa wa Kitinye na Jacob Chacha Mwita ambaye ni Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kitinye.

Aprili 8,2024 washitakiwa hao katika Mahakama ya Wilaya Ilala mbele ya Mhe. Aneth Nyenyema-Hakimu Mkazi Mwandamizi wamefunguliwa Shauri la Uhujumu Uchumi namba 9069/2024.

Ilidaiwa walitenda hayo kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sura ya 329 marejeo ya Mwaka 2022 ikisomwa pamoja na Aya ya 21 ya Jedwali la kwanza na vifungu vya 57(1) na 60(2) vya Sheria ya Uhujumu Uchumi sura 200 marejeo ya 2022 na Sheria ya Kuzuia Utakatishaji fedha, Sura ya 423 marejeo ya Mwaka 2022.

Hata hivyo,washtakiwa wote walikana makosa yao na kupelekwa rumande baada ya kutotimiza vigezo vya dhamana kwa mshtakiwa Eric Isack Gabriel,Sabina William Ndasi na Jacob Chacha Mwita

Aidha, Mshtakiwa Sefania Adam Mwanja hakupewa dhamana kwa kuwa ana shtaka la utakatishaji fedha ambalo halina dhamana kisheria.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 22, 2024 kwa ajili ya kusoma hoja za awali.

Msingi wa shauri hilo ni udanganyifu katika uundwaji wa kikundi ambacho kilipewa mkopo wa shilingi milioni 100.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news