Mkusanya mapato Muleba hatiani kwa hongo

KAGERA-Mahakama ya Wilaya Muleba mkoani Kagera imemhukumu,Bw. Alexander Mathias Rugema ambaye ni mkusanya mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Muleba kwa njia ya POS.
Mshtakiwa ametiwa hatiani na kuamriwa alipe faini ya shilingi 500,000 au jela miaka miwili.

Ni kwa kujipatia manufaa ya shilingi 2,074,500 kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329.

Hukumu hiyo dhidi ya Bw. Alexander Mathias Rugema katika Kesi ya Jinai namba 9168/2024 imetolewa Aprili 8,2024 chini ya Mhe. Lilian Mwambeleko ambaye ni Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Muleba.

Ilidaiwa kwamba, mshtakiwa akiwa Mkusanya Mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Muleba kwa njia ya POS, alishtakiwa kwa kosa la hongo na kujipatia manufaa yasiyostahili.

Ni wakati wa ukusanyaji wa maduhuri ya Serikali, hivyo kufanya upotevu wa shilingi 2,074,500 mali ya Halmashauri ya Muleba.

Mshtakiwa amelipa faini mahakamani ya shilingi 500,000 na kutanguliza sshilingi 810,000 kama fedha alizojinufaisha nazo kwa kujutia kosa lake, na mahakama imemuamuru kukamilisha fedha zote zilizobaki ndani ya miezi mitatu na kuachiwa huru.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news