Waziri wa Fedha ateta na uongozi wa USAID


Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) ukiongozwa na Msaidizi wa Utawala anayesimamia Afrika, Dkt. Monde Muyangwa, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na Tanzania.
Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Shirika hilo, jijini Washington D.C, nchini Marekani na kuhudhuriwa pia na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bw. Lawrence Mafuru na Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania- TRA, Bw. Mcha Hassan Mcha.
Ushirikiano wa Tanzania na Marekani umetimiza zaidi ya miaka 50 ambapo makubaliano ya kwanza ya kuanzishwa kwa uhusiano huo yalisainiwa mwaka 1968.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news