Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Mei 27,2024

TANGA-Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake Taifa ya Chama cha ACT-WAZALENDO, Janeth Rithe amelaani kitendo cha Mkuu Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Paul Makonda kumdhalilisha mtumishi mwanamke. Akizungumza katika uwanja wa Soko la Ngamiani jijini Tanga mwishoni mwa wiki,Janeth amemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kumchukulia hatua Paul Makonda.


"Ukiona kifaranga cha kuku kiko juu ya chungu yuko mama yake chini, lawama hizi tunampelekea Mama Samia, yeye ndiye mteule anayeteua wakuu wa mikoa, anayeteua wakuu wa mikoa halafu Mwenyekiti wa Wanawake (UWT) anatoka hadharani kulialia na kulalamika, haya ndiyo malezi ya Chama Cha Mapinduzi namna walivyowalea vijana wao.

"Wamekosa adabu, wamemkosa nidhamu ni sawasawa na ukoo wa kambale,baba ana ndefu, mtoto ana ndefu, mjukuu ana ndefu hicho ndiyo Chama Cha Mapinduzi, sasa udhalilishaji anaofanya Makonda sababu ni Samia Suluhu Hassan kama anaweza amchukulie hatua, wakati wa kulia na kulalamika umekwisha.Sasa kama tuna viongozi wanawake, jukumu lao ni kulia, hii nchi itaonewa jamani," amesisitiza Rithe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news