Mabasi 10,270 na vichwa 20 vya treni vinafuatiliwa kupitia Mfumo wa VTS

NA GODFREY NNKO

KATIKA kudhibiti mwenendo wa mabasi ya masafa marefu na treni, Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeendelea kufuatilia mwenendo wa mabasi na vichwa vya treni kupitia Mfumo wa Ufuatiliaji wa Mwenendo wa Vyombo (Vehicle Tracking System-VTS).

Hadi kufikia Machi, 2024 mabasi 10,270 yanayotoa huduma ya usafiri wa masafa marefu na vichwa vya treni 20 ambavyo vimegawanyika TAZARA 18 na TRC viwili vimeunganishwa katika mfumo huo. Hayo yamesemwa leo Mei 6,2024 na Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Prof.Makame Mbarawa wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.

Amesema, matumizi ya mfumo huo yamepunguza ajali zitokanazo na mwendokasi na kuongeza ufanisi wa vyombo vinavyodhibitiwa.

Waziri Prof.Mbarwa amebainisha kuwa,kwa mwaka 2022/23 ajali zilipungua hadi kufikia ajali 166 za mabasi ya masafa marefu ikilinganishwa na ajali 179 zilizotokea mwaka 2021/22. 12.

"Mheshimiwa Spika, utakumbuka kuwa, tarehe 28 Juni 2023, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alitangaza hapa Bungeni uamuzi wa Serikali wa kuondoa zuio la mabasi ya abiria kusafiri nyakati za usiku lililowekwa mwaka 1994.

"Napenda kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi na LATRA ilifanya maandalizi na kuanza kutoa ratiba za mabasi kusafiri nyakati za usiku kuanzia tarehe 1 Oktoba, 2023."

Amesema,hadi kufikia Machi, 2024 jumla ya ratiba za mabasi 798 zimetolewa kwa ajili ya safari za usiku.

"Ni dhahiri kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeonesha dhamira ya kweli ya kuifungua nchi kiuchumi."

Ombi

Waziri Prof.Mbarwa katika mwaka wa fedha 2024/25, ameliomba Bunge kuidhinisha jumla ya shilingi trilioni 2.73 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Amesema, kati ya fedha hizo, shilingi 114,744,476,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 2.6 ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news