MWANZA-Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Prof.Najat Kassim Mohammed amehitimisha ziara yake ya kutembelea ofisi za Kanda ya Ziwa kuzungumza na wadau wanaoshirikiana na TAEC.

Sambamba na kuzungumza na wafanyakazi wa TAEC ili kujua mafanikio na changamoto wanazopitia katika kutekeleza majukumu yao.
Prof. Najat ametembelea vituo sita ambavyo ni Kituo cha TARI-Ukiliguru, Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Uwanja wa Ndege jijini Mwanza, Bandari ya Mwanza, Ofisi ya Makao Makuu ya Kanda ya Ziwa iliyopo Nyegezi jijini Mwanza pamoja na Ofisi ya TAEC mpakani Sirari mkoani Mara.
