Rais Dkt.Samia, Nyusi watembelea banda jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zake

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama wakati akitoa maelezo kuhusu Mfumo wa Ufuatiliaji wa mwenendo wa majanga na tahadhari ya mapema (MYDEWETRA) wakati walipotembelea katika Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizochini yake katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) leo Julai 3 2024 jijini Dar es Salaam.
Maonesho hayo ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam (Sabasaba) yamefunguliwa rasmi leo (Julai 3, 2024) na Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi pamoja na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news