Wafanyabiashara 891 warejeshwa Soko la Kariakoo

NA GODFREY NNKO

SHIRIKA la Masoko ya Kariakoo limetoa orodha ya wafanyabiashara 891 waliokidhi vigezo vya kurejeshwa kufanya biashara katika Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo lililopo jijini Dar es Salaam.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Julai 10,2024 na Menejimenti ya shirika hilo ambayo imefafanua kuwa, uamuzi huo umefikiwa baada ya mradi wa ujenzi wa soko jipya na ukarabati kukamilika.

"Wafanyabiashara wanaodaiwa na shirika ambao wapo kwenye orodha hii wanajulishwa
kuwa hawatarejeshwa sokoni hadi watakapolipa madeni ya kodi waliyolimbikiza kwa muda mrefu.

"Shirika linatoa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia leo tarehe 10 Julai 2024 hadi tarehe 09 Agosti 2024 kwa wadaiwa wote kukamilisha malipo ya madeni yao.

"Kwa wafanyabiashara wenye hoja au maoni kuhusu majina yao kutoonekana kwenye orodha ya uhakiki, shirika linatoa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 11 hadi 13 Julai 2024 kuwasilisha madai yao.

"Maafisa wa shirika watakuwepo katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 9.00 alasiri
kusikiliza na kutoa ufafanuzi kwa wafanyabiashara."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news