REA yawapa wanafunzi darasa kuhusu Nishati Safi ya Kupikia

DODOMA-Wanafunzi kutoka Shule za Sekondari Itega na Lukundo wamevutiwa na Banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) hususan teknolojia ya kisasa ya Nishati Safi ya Kupikia.Wakizungumza kwa nyakati tofauti Agosti 6, 2024 walipotembelea Banda la REA wanafunzi hao walisema wamehamasika kushuhudia mambo makubwa yanayofanywa na Serikali hususan katika kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia pamoja na namna ambavyo Serikali imejizatiti kupeleka maendeleo maeneo ya vijijini.
"Tumejifunza kuhusu teknolojia ya kisasa na matumizi ya Nishati Safi ya kupikia ambayo imelenga kuboresha mazingira. Hii imetuongezea uelewa kwa yale tunayofundishwa shuleni," amesema Irene Robert, Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza Sekondari ya Itega.
"Tumefurahi sana, Serikali yetu inafanya mambo makubwa kwa wananchi wake, tumeona namna ambavyo REA imesambaza umeme maeneo ya Vijijini na harakati zingine za kimaendeleo tuliyoelezwa hapa," amesema Baraka Elikana, Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza Lukundo Sekondari.
Wanafunzi hao wamekiri kuondoka na elimu ambayo hawakuwa nayo hapo awali kabla ya kutembelea Banda la REA.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news