Serikali yawataka wananchi kutumia elimu ya fedha ipasavyo

FARIDA RAMADHANI
NA JOSEPH MAHUMI

WAKAZI wa Jiji la Mbeya wametakiwa kutumia elimu waliyoipata katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Kitaifa kubadilisha maisha yao hususan katika masuala ya usimamizi wa fedha.
Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja, akizungumza wakati akifunga rasmi Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yaliyofanyika katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yalizikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Mbeya na mikoa jirani.

Rai hiyo imetolewa na Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja, wakati akifunga maadhimisho hayo Jijini Mbeya.

Dkt. Mwamwaja alisema kwamba elimu waliyoipata inatakiwa iwabadilishe kwa kuacha mambo yote waliyokuwa wakiyafanya awali kwa kufuata utaratibu na maamuzi sahihi wanaposhighulikia masuala yao ya kifedha.
Baadhi ya Washiriki na Wananchi wa Jiji la Mbeya, wakifuatilia hotuba ya Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja (hayupo pichani) wakati akifunga rasmi Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yaliyofanyika katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yalizikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Mbeya na mikoa jirani.

“Wataalam wanasema mikopo siyo mibaya, lakini kabla hujakopa lazima uwe na malengo, usikope kwa sababu fedha zipo mahala fulani, ukope ukiwa na mpango. Naamini hii ni sehemu mojawapo ya kubadilika”, alisisitiza Dkt. Mwamwaja.

Alisisita wananchi wanapochukua mikopo wahakikishe wanasoma mikataba na kuchukua nakala za mikataba hiyo ili kuepuka madhara mbalimbali yanayotokana na mikop yenye masharti magumu maarufu kama mikopo umiza.
Meza kuu ikiongozwa na Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja (Katikati aliyeketi), wakiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yaliyofanyika katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yalizikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Mbeya na mikoa jirani.

Dkt. Mwamwaja pia alitoa rai kwa wananchi hao kutumia huduma rasmi za fedha kwa kuhakikisha kila wanachokifanya katika shughuli zao za masuala ya kifedha ziwe zimerasimishwa.

“Kama ni kikoba ni jambo zuri na kinaungwa mkono lakini hicho kikoba kisajiliwe ili kiwe rasmi,”aliongeza Dkt. Mwamwaja.
Meza Kuu ikiongozwa na Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja (Katikati aliyeketi), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki kutoka taasisi mbalimbali wa Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yaliyofanyika katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yalizikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Mbeya na mikoa jirani

Aliwasihi kutumia elimu waliyoipata kuwaelimisha wengine ambao hawakuweza kufika katika maadhimisho hayo kwa kuwa elimu ya fedha ni endelevu na haitolewi kwenye maadhimisho hayo pekee.

Aidha, alisema utoaji wa elimu ya fedha ni endelevu ingawa utoaji wa elimu hiyo kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa hutolewa mara moja kwa mwaka.

“Maadhimisho haya ambayo tunamaliza leo sio mwisho wa kutoa elimu, bado tutaendelea na kutumia njia mbalimbali katika kutoa elimu ya fedha, tusitoke hapa tukasema baada ya maadhimisho haya fursa hii ya kutoa elimu inafungwa hadi mwakani, Hapana. Utoaji wa elimu ya fedha ni endelevu,”alisema Dkt. Mwamwaja.
Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja (kushoto) akimkabidhi zawadi Mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mkapa, Bless Mwamkinga, baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika Shindano la Uandishi wa Insha kuhusu elimu ya fedha, wakati wa hafla ya kufunga rasmi Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yaliyofanyika katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yalizikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Mbeya na mikoa jirani. Kushoto ni Meneja Uendeshaji Bodi ya Bima ya Amana (DIB), Bw. Nkanwa G. Magina.
Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja, akimkabidhi Tuzo, Afisa Utafiti na Mawasiliano wa Umoja wa Mabenki (Tanzania Bankers Assosication – TBA), Bi. Sophia Mmbuji baada ya TBA kuibuka mshindi wa uhamasishaji bora wa maadhimisho katika vyama vilele kwa uratibu wa taasisi zao na kufanikisha ushiriki kwa zaidi ya asilimia 50, wakati wa hafla ya kufunga rasmi Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yaliyofanyika katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yalizikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Mbeya na mikoa jirani.
Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja, akimkabidhi Tuzo, Mkuu wa Kitengo cha Habari, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Bw. Ibrahim Hamidu baada ya kuibuka ushindi wa uhamasishaji bora wa maadhimisho katika Usimamizi wa Sekta ya Fedha na kuhamasisha ushiriki wa taasisi zao kwa kiwango cha kuanzia asilimia 50, wakati wa hafla ya kufunga rasmi Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yaliyofanyika katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yalizikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Mbeya na mikoa jirani.
Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja, akimkabidhi Tuzo Afisa Mikopo wa Hazina Saccoss, Bi. Bakhita Malongo, baada ya taasisi hiyo kuibuka na ushindi wa mtoaji huduma bora za fedha katika kipengele cha Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo (SACCOSS), wakati wa hafla ya kufunga rasmi Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yaliyofanyika katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yalizikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Mbeya na mikoa jirani.
Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja, akimkabidhi Tuzo Afisa Uhusiano na Elimu kwa Umma Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Bi. Stella John, baada ya Mamlaka hiyo kuibuka mshindi wa uhamasishaji bora wa maadhimisho katika Usimamizi wa Sekta ya Fedha na kuhamasisha ushiriki wa taasisi zao kwa kiwango cha kuanzia asilimia 50, wakati wa hafla ya kufunga rasmi Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yaliyofanyika katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yalizikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Mbeya na mikoa jirani.
Alisema Serikali kupitia Wizara ya Fedha imeteua Waratibu wa Huduma Ndogo za Fedha katika kila mkoa na halmashauri nchini ambao wamekuwa wakitoa elimu ya fedha kwa wananchi.

Maadhimisho hayo ni ya nne kufanyika nchini ambayo ni utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha wa Mwaka 2020/21 – 2029/30 na yanalenga kutoa elimu ya fedha kwa umma na kuongezeka kwa mchango wa Sekta ya Fedha kwenye ukuaji wa Uchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news