ONTARIO-Kampuni ya Dhahabu ya Barrick (NYSE:GOLD)(TSX:ABX) imepokea kwa furaha uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Ontario wa kutupilia mbali madai yaliyotolewa na wakazi wa Tanzania waliokuwa wakilalamikia ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na askari wa Jeshi la Polisi Tanzania jirani na mgodi wa dhahabu wa kampuni hiyo wa North Mara.
Mahakama hiyo iliamua kwamba Ontario haikuwa jukwaa mwafaka la kusikiliza madai hayo.Rais na Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow, alisema kampuni hiyo imekanusha mara kwa mara kile inachokiona kama madai yasiyo na msingi yanayotolewa asasi chache zisizo za serikali zenye mrengo wa kianaharakati zinaodai kuwapo kwa ukiukwaji wa kihistoria wa haki za binadamu katika maeneo yanayozunguka mgodi wake wa North Mara.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo