Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yaendesha mafunzo ya Mfumo wa SEMA NA BoT

DAR-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa mafunzo maalum kwa mabenki, watoa huduma ndogo za fedha na watoa huduma za kifedha kwa njia za mtandao kuhusu Mfumo wa Kushughulikia Malalamiko ya Wateja wa Huduma za Fedha (Financial Complaints Resolution System) ambao umetengenezwa na BoT. Mafunzo hayo yamefanyika kuanzia tarehe 8 hadi 11 Aprili, 2025, katika ofisi za BoT jijini Dar es Salaam, yakilenga kuwajengea uwezo washiriki hao kuhusu namna ya kushughulikia malalamiko ya wateja kwa ufanisi, usawa na haki.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha wa BoT, Bw. Kennedy Komba, amesema mfumo huu unaoitwa SEMA NA BoT unakusudia kulinda haki za wateja na watoa huduma za fedha kwa lengo la kuimarisha sekta hiyo.
"Mfumo huu utasaidia kuhakikisha haki za wateja na watoa huduma za fedha zinalindwa, utatuzi wa malalamiko unafanyika kwa wakati na kwa usawa, utapandisha hadhi ya watoa huduma za fedha na kujenga imani ya wateja kwa watoa huduma hao,” amesema Bw. Komba.

Ameongeza kuwa uwepo wa mfumo utasaidia katika mamlaka za usimamizi wa sekta ya fedha katika uundaji wa sera na miongozo mbalimbali ya kuboresha utendaji wa sekta hiyo.

Aidha, ameeleza kuwa mfumo huu utawezesha mawasiliano ya moja kwa moja kati ya wateja, watoa huduma za fedha na BoT kupitia njia mbalimbali za teknolojia ya mawasiliano ikiwemo tovuti (web application), misimbo ya USSD, na simu (mobile app).
Mkurugenzi huyo amebainisha pia kuwa Benki Kuu itaimarisha zaidi mfumo wa SEMA NA BoT ili kuzidi kurahisisha utatuzi wa malamiko ya wateja.

“Tuna mpango wa kuimarisha zaidi mfumo huu kwa kuongeza teknolojia ya kisasa ya Akili Unde (AI), kama vile Chatbot, pamoja na Mfumo wa Kujibu Maswali kwa Njia ya Sauti (IVR) ili kurahisisha mchakato wa utatuzi wa malalamiko.”

Kwa upande wake, Bw. Innocent Massawe, mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo amesisitiza kuwa mfumo huu utaongeza uwajibikaji kwa taasisi za fedha kupitia kushughulikia malalamiko ya wateja kwa wakati na usawa.

“Mfumo utaongeza uwajibikaji kwa taasisi za kifedha katika kuhakikisha kwamba wanashughulikia malalamiko yanayowasilishwa na wateja kwa usawa, uwazi na haki kitu ambacho kitachangia watoa huduma kubakisha wateja wao ambao wangeweza kuwapoteza kutokana na kutoridhishwa na huduma,” ameeeleza.
“Mfumo utaongeza uwajibikaji kwa taasisi za kifedha katika kuhakikisha kwamba wanashughulikia malalamiko yanayowasilishwa na wateja kwa usawa, uwazi na haki kitu ambacho kitachangia watoa huduma kubakisha wateja wao ambao wangeweza kuwapoteza kutokana na kutoridhishwa na huduma,” ameeeleza.

Aidha, washiriki hao wapatao 200 wameipongeza Benki Kuu kwa jitihada mbalimbali inazofanya katika kuimarisha sekta ya fedha nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news