Dkt.Nchemba afanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la UN Women

DAR-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Usawa wa Jinsia (UN Women), Bi. Hodan Addou, Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadili masuala ya ushirikiano kati ya Shirika hilo na Tanzania hususan katika kuwawezesha wanawake kupitia Bajeti Kuu ya Serikali.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Kamisha wa Idara ya Sera Wizara ya Fedha, Dkt. Johnson Nyella, Kamishna Msaidizi kutoka Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Robert Mtengule na maafisa wengine waandamizi wa Serikali na Shirika hilo la UN Women.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news