DODOMA-Serikali kupitia Wizara ya Madini imetunga kanuni za msaada wa kiufundi katika Leseni ndogo za uchimbaji wa Madini ambapo zitaratibu ushiriki wa wageni katika Leseni ndogo za uchimbaji wa Madini (PML) ambazo kwa mujibu wa kifungu cha 8 cha Sheria ya Madini sura ya 123,kimezitamka Leseni hizi kama maalum kwa ajili ya Watanzania












