Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) laomboleza kifo cha Papa Francis

DAR-Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limesema limepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Kiongozi wa Kanisa Katoliti Duniani, Baba Mtakatifu Papa Francis aliyefariki dunia siku ya Jumatatu tarehe 21 Aprili,2025 akiwa na umri wa miaka 88.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile amebainisha kuwa, katika kipindi chote cha miaka 12 akiwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Papa Francis atakumbukwa kwa juhudi zake za kuhimiza mazungumzo kati ya dini mbalimbali,utetezi wa wanyonge, na msimamo wake thabiti katika kulinda utu wa mwanadamu, pamoja na kudumisha amani.

"TEF inatoa pole za pekee kwa Balozi wa Vatican nchini Tanzania,Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na waumini wote wa Kanisa Katoliki hapa nchini na duniani kote. ikiwaombea faraja,subira na nguvu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na maombolezo;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news