Muhimu:Kuondolewa kwa zuio la mazao ya kilimo kuingia nchini kutoka Malawi na Afrika Kusini

DODOMA-Wizara ya Kilimo imetangaza kuondoa mazuio yote ya biashara na usafirishaji wa mazao yaliyowekwa na Tanzania kwa nchi za Malawi na Afrika Kusini kuanzia leo April 26, 2025 kwa kile ambacho Serikali inaamini majadiliano yanayoendelea
yataleta suluhisho.

“Serikali kupitia Wizara ya Kilimo ilitangaza tarehe 23 Aprili 2025, kuzuia mazao kutoka nchi za Afrika Kusini na Malawi kuingia katika mipaka ya Tanzania hadi hapo hatua zitakapochukuliwa kwa nchi hizo kuruhusu mazao yetu kuingia katika masoko yao, kufuatia zuio hilo, Serikali za Malawi na Afrika Kusini zimewasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Kilimo za Tanzania ili kuweza kutafuta suluhisho la zuio husika”

“Kuhusu zuio la Afrika Kusini, majadiliano ya Wataalamu wa Wizara ya Kilimo kupitia Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania yanaendelea kwa pamoja na Mamlaka za nchi ya Afrika Kusini zinazohusiana na Afya ya Mimea na Masoko.”

“Serikali inawahakikishia wakulima na wananchi wa Tanzania kwa ujumla kuwa, uhuru wa biashara ya mazao ya kilimo kulingana na matakwa ya afya ya mimea, rasilimali za nchi zilizopo na mahusiano mapana ya kidiplomasia kwa faida ya wote;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news