Rais Dkt.Mwinyi ajumuika na wananchi katika ibada,kuzifariji familia zilizoondokewa na wapendwa wao

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Taubat , Michungwa Miwili uliopo Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Baada ya Sala ya Ijumaa, Rais Dkt.Mwinyi aliwaongoza waumini katika Sala ya Maiti ya Marehemu Haroub Muhammed Kassim aliyefariki jana iliyofanyika msikitini hapo na baadae kuifariji familia nyumbani kwa marehemu na kuwataka kuwa na subira wakati huu wa msiba huo mzito.
Wakati huohuo Rais Dkt.Mwinyi alitoa mkono wa pole kwa familia mbili zilizofiwa hivi karibuni. .
Familia hizo ni ya marehemu Kanali Masoud Khamis ya Mitiulaya pamoja na Familia ya Marehemu Mzee Haji Machano ya Kikwajuni Majabalini aliyekuwa Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news