Rais Dkt.Mwinyi ajumuika na wananchi katika mazishi ya marehemu Sanya

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na wananchi katika mazishi ya marehemu Muhammad Ibrahim Sanya yaliofanyika leo.
Rais Dkt.Mwinyi aliwaongoza waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Maiti katika Msikiti Jibril Mkunazini Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 22 Aprili 2025.
Marehemu Ibrahim Sanya amefariki jsna wakati akitibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Wa Mjini Magharibi Lumumba.

Wakati wa uhai wake marehemu Ibrahim Sanya aliwahi kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Jimbo la Mkunazini kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF).
Marehemu Sanya amezikwa eneo la Makaburi ya Kijitoupele Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news