LONDON-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemshukuru Waziri Mkuu mstaafu wa Uingereza ambaye pia ni Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Tony Blair Institute for Global Change (TBI), Sir Tony Blair kwa ushirikiano wake katika sekta mbalimbali ikiwemo kuimarish bandari, utalii na kuwajengea uwezo Taasisi ya Ufuatiliaji na Usimamizi wa Serikalini (PDB).
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo leo Aprili 6,2025 alipozungumza na Waziri Mkuu Mstaafu huyo, alipomtembelea kwenye makazi yake The South Pavillion, Cotton Underwood Aylesbury, Uingereza.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amemhakikishia kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu utafanyika kwa amani na utulivu katika kuendeleza Serikali ya Umoja wa Kitaifa.Naye Waziri Mkuu mstaafu Tony Blair amemuahidi Rais Dkt.Mwinyi kuendelea kushirikiana na Zanzibar katika uchumi wa kidigitali,utalii,uwekezaji kupitia taasisi yake ya TBI.

