HELSINKI-Rais wa Jamhuri ya Finland, Mheshimiwa Alexander Stubb na mkewe Suzanne Innes-Stubb wanatarajia kufanya ziara ya kiserikali ya siku tatu kuanzia Mei 14 hadi 16,2025 nchini Tanzania.
Stubb ambaye ni Rais wa 13 wa Taifa hilo la Ulaya Kaskazini anafanya ziara hiyo ya kwanza Tanzania ikiwa ni ndani ya mwaka mmoja wa uongozi wake tangu aingie madarakani, 2024.
Kabla ya kuwa Rais aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Finland kuanzia mwaka 2014 hadi 2015.
Pia, ziara hiyo ni sehemu ya kusherehekea miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Finland.