ZANZIBAR-Chuo Kikuu Cha Taifa Zanzibar (SUZA) kimepokea ripoti ya utekelezaji ya ujenzi wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi (HEET).
Ripoti hizo zimewasilishwa jana na kampuni ya ujenzi ya Mohammed Builder iliwemo ya utekelezaji wa ujenzi uliofikia asilimia 28, pamoja na taarifa ya masuala ya mazingira na usalama kwa jamii.
Aidha, walioshiriki wengine ni wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Tanzania, kampuni ya Ushauri Elekezi ya Arqes Afrika pamoja na watekelezaji wa Mradi wa HEET wa Chuo cha SUZA.









