Tanzania imejifunza mengi Mradi wa Chaguo Langu Haki Yangu-Katibu Mkuu Abeida

DAR-Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar,Bi. Abeida Rashid Abdallah amesema,Tanzania kwa ujumla imejifunza mengi kutokana na Mradi wa Chaguo Langu Haki Yangu.

Mradi huo umelenga utetezi wa haki na uchaguzi wa wanawake na wasichana wenye ulemavu,kuhakikisha zinalindwa na kuimarishwa kupitia njia mbalimbali ambazo wanakabiliana nazo ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia (GBV) na mila potofu.
Bi.Abeida ameyasema hayo katika mkutano wa kutathmini utekelezaji wa mradi wa Chaguo Langu Haki Yangu (My Choice My Right) uliofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton jijini Dar es Salaam.

Amesema, mafanikio yaliyopatika kapitia mradi huo yanaweza kuisogeza Tanzania katika kuyafikia Malengo ya Maendelo endelevu (SDGs) ifikapo mwaka 2030.

Ameeleza kwamba, katika utekelezaji wa mradi huo, mafanikio kadhaa yamepatikana ikiwemo kuimarika kwa mifumo ya kijamii ya kupambana na vitendo vya ukatili na udhalilishaji, ndoa za utotoni, kuimarika kwa Sera na Miongozo ya kukabiliana na vitendo vya ukatili na udhalilishaji.

Pia,kuongezeka kwa ushiriki wa Watu Wenye Ulemavu katika mapambano ya vitendo vya ukatili na udhalilishaji.
Amefafanua kuwa, mradi huo umefadhiliwa na Serikali ya Finland kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi (UNFPA) ambapo umetekelezwa kwa kipindi cha miaka minne (2021-2024).

Ni katika wilaya sita za Tanzania Bara na Zanzibar ikiwemo Wilaya ya Chake Chake Pemba,Wilaya Mjini katika Mkoa wa Mjini Magharib Unguja, Wilaya Shinyanga, Tarime, Butiama, Kishavu na umegharimu fedha za Tanzania Tsh. Bilioni 13.1.
“Mafanikio hayo ambayo yameelekezwa moja kwa moja kwa wanawake na wasichana wakiwemo wanawake na wasichana wenye ulemavu ni msaada mkubwa kwa utekelezaji Sera na Mikakati ya Zanzibar katika kukabiliana na vitendo vya ukatili na udhalilishaji kama ilivyoainishwa katika Mpango Kazi wa Kupambana na Udhalilishaji wa Wanawake na Watoto (NPA-VAWC II 2025-2030),”alisema Katibu Mkuu huyo.

Aidha,Katibu Mkuu huyo ametoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Finland, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi (UNFPA) kwa kutekeleza mpango huo kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania na wadau wa asasi za kiraia kwa lengo la pamoja la kuhamasisha upatikanaji wa haki za wanawake na wasichana katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sambamba na hayo ameiomba Serikali ya Finland iendelee kushirikiana na Shirika la UNFPA kuisaidia Serikali ya Tanzania kufikia Wilaya zote kupitia awamu nyingine ya mradi kama huo ili nchi iweze kufikia malengo ya kuishi katika jamii isiyo na udhalilishaji, ubaguzi kwa wanawake na wasichana wakiwemo wanawake na wasichana wenye ulemavu.

Naye Mratibu wa Mradi Chagua langu haki Yangu ndugu Rashida Sharif amesema kupita mradi huo Watu Wenye Ulemavu wamepata fursa ya kupaza sauti zao kueleza changamoto zinazowakabili ili Serikali ichukuwe hatua mbali mbali za kuzitatua ili waishi kwa furaha na amani katika nchi.
Kwa Upande wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar Ndugu Ussi Khamis Debe amesema Watu Wenye Ulemavu wamefaidika kwani UNFP wamekua na Mfumo Jumuishi wa Watu Wenye Ulemavu ambapo itawasaidi katika mipango yao hasa katika masuala ya elimu, Afya na Uchumi.

Akizungumza moja kati ya walengwa wa Mradi kutoka Shinyanga Maryam Mbarouk amesema kabla ya mradi kuanza hakua na ujuzi wowote lakini kupitia Mradi huo amepelekwa Chuo cha Ufundi VETA, Hivyo amepata elimu na vifaa vya kuanza kazi ya ujasiriamali hatimae ameanzisha kikundi ambacho kimewashirikisha wanawake wenyeulemavu na wasiokua na ulemavu wameanzaa kunuafaika na elimu ya ufundi stadi na lifu skili (life Skill).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news