KIGALI-Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Tanzania, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, amesema Tanzania imeongeza kasi katika kutumia na kuendeleza teknolojia ya Akili Unde (Ai) katika elimu kupitia utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Matumizi ya Teknolojia za Kidijitali.

“Tanzania imeongeza kasi ya matumizi ya teknolojia za kidijitali ambayo ni dhamira ya Serikali ya Tanzania ya kuwawezesha vijana kupata mafunzo ya akili bandia na teknolojia zinazoibukia kupitia ufadhili wa masomo katika vyuo vikuu bora duniani.”
Prof. Mkenda amesema kuwa Serikali pia imeboresha Sera ya Taifa ya Elimu na Mafunzo pamoja na mitaala, kwa lengo la kuanza kuwajengea vijana uwezo wa TEHAMA ikiwemo Coding, kuanzia ngazi za chini za elimu
Mjadala huo pia ulihusisha washiriki mashuhuri wakiwemo Waziri wa Elimu wa Rwanda, Mhe. Joseph Nsengimana, Mkurugenzi wa Uchumi wa Kidijitali kutoka Mastercard Foundation, pamoja na wawakilishi kutoka China na sekta binafsi.