SINGIDA-Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mheshimiwa Halima Dendego anatarajiwa kuzindua Kamati ya Ushauri wa Kisheria ngazi ya Mkoa na Wilaya na Kliniki ya Sheria bila Malipo Mkoa wa Singida. Hafla ya uzinduzi huo itafanyika Mei 19,2025 katika Viwanja vya Stendi ya zamani ya Manispaa ya Singida.