MAPUTO-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji ambaye pia anawakilisha mataifa ya Madagascar na Eswatini,Mheshimiwa CP Hamad Khamis Hamad ameshiriki kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Afrika zilizofanyika Jijini Maputo, Msumbiji leo Mei 25,2025.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji anayewakilisha pia Madagascar na Eswatini,Mheshimiwa CP Hamad akiteta jambo na Balozi wa Misri nchini Msumbiji, Mheshimiwa Mohamed Hassan Rafaat Aly Farghal.
Mheshimiwa Balozi Hamad akiwa na Balozi wa Jamhuri ya Kenya nchini Msumbiji, Mheshimiwa Philip Mundia Githiora (kulia) na Balozi wa Jamhuri ya Rwanda nchini Msumbiji, Mheshimiwa Donat Ndamage (kushoto).Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Viongozi wengine Waandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Msumbiji akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa nchi hiyo, Mhe. Balozi Maria Manuela dos Santos Lucas na Mabalozi wa Afrika wanaoziwakilisha nchi zao nchini Msumbiji.


