Dkt.Biteko awasili nchini Morocco kwa ziara ya kikazi

RABAT-Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili nchini Morocco kwa ziara ya kikazi inayolenga kukuza na kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizi mbili katika Sekta ya Nishati.
Mara baada ya kuwasili, Dkt. Biteko amepokelewa na Naibu Waziri wa Mageuzi ya Nishati na Maendeleo Endelevu nchini humo, Mhe. Mohamed Ouhmed, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na mwakilishi katika eneo la Morocco, Mhe. Ali Jabir Mwadini.
Akiwa nchini humo, Dkt. Biteko anatarajiwa kukutana na kuzungumza na mwenyeji wake Waziri wa Nishati na Maendeleo Endelevu wa Ufalme wa Morocco, Mhe. Leila Benali ambapo watajadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Nishati.
Dkt. Biteko ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Dennis Londo, Wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa nishati vijijini (REA), Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news