DAR-Washiriki wa Shule ya 13 ya Kanda ya Afrika kuhusu Usimamizi wa Mtandao (AfriSIG) kutoka katika nchi za Afrika ikiwemo Tanzania wakiendelea na darasa lililoanza leo Mei 24 na linatarajiwa kuhitimishwa Mei 28, 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Tume ya TEHAMA (ICTC), Dk. Nkundwe Moses Mwasaga, akifungua rasmi mafunzo ya muda mfupi ya Shule ya 13 ya Kanda ya Afrika kuhusu Usimamizi wa Mtandao (AfriSIG) yanayofanyika tarehe 24 hadi 28 Mei, 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Shule hiyo imeandaliwa na Chama cha Mawasiliano kwa Maendeleo (APC), Idara ya Jamii ya Habari ya Tume ya Umoja wa Afrika (AUC), na Taasisi ya Utafiti wa ICT Afrika (RIA), kwa kushirikiana na Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi kwa Afrika (UNECA) na Mchakato wa Kibunge wa Jukwaa la Umoja wa Mataifa la Usimamizi wa Mtandao.
Picha za pamoja za washiriki wa mafunzo ya muda mfupi ya Shule ya 13 ya Kanda ya Afrika kuhusu Usimamizi wa Mtandao (AfriSIG) kutoka katika nchi za Afrika ikiwemo Tanzania wakiwa na Dk. Nkundwe Moses Mwasaga, Mkurugenzi wa Tume ya TEHAMA (ICTC) mara baada ya kufungua mafunzo ya shule hiyo tarehe 24 Mei, 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa mafunzo ya muda mfupi ya Shule ya 13 ya Kanda ya Afrika kuhusu Usimamizi wa Mtandao (AfriSIG) wakichangia na kujadili kuhusu mada ya usimamizi wa mtandao na usimamizi wa data leo tarehe 24 Mei, 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
























