Dubai kuchangisha shilingi milioni 150 za kununua gari la kwaya



NA RESPICE SWETU

JUMLA ya shilingi milioni mia moja na hamsini zinatarajiwa kukusanywa katika harambee ya kuchangia ununuzi wa basi la kwaya ya Mtakatifu Andrea kanisa kuu la Anglikana la mjini Kasulu.
Akizungumza kuhusu harambee hiyo mwenyekiti wa kwaya Anania Mbango amesema, maandalizi yote kuelekea harambee hiyo yamekamilika.

Ameongeza kuwa, harambee hiyo inayotarajiwa kuwa kubwa kuliko zote zilizofanyika mjini Kasulu, itafanyika kwenye viwanja vya ofisi ya Askofu mkuu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Western Tanganyika Jumapili Juni Mosi, ikitanguliwa na misa itakayoongozwa na Askofu mkuu wa kanisa hilo Emmanuel Bwata.

Mfanyabiashara mzawa wa Kasulu Evance Chocha Bachunya maarufu kwa jina la Dubai, anatarajiwa kuongoza harambee hiyo sambamba na wafanyabiashara wengine maarufu kutoka ndani na nje ya wilaya ya Kasulu.“Tumewaalika pia viongozi wa serikali, asasi, mashirika na taasisis mbalimbali za umma kwenye harambee hiyo,”amesema Mbango.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka katika kamati ya maandalizi ya harambee hiyo, Dubai ambaye pia ni mkurugenzi wa Bwami Dubai Hoteli, anatarajiwa kuwasili mjini Kasulu Alhamis Mei 29.

Kuhusu matumizi ya basi hilo Mbango amesema, pamoja na kutumiwa na wana kwaya kwenye safari za uinjilishaji, basi hilo pia litakuwa ni sehemu ya kitega uchumi cha kwaya hiyo kwa kulikodishwa katika matumizi mbalimbali.

Mwenyekiti wa kwaya hiyo ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya maandalizi, amewaalika wakazi wa Kasulu kujitokeza kwa wingi katika tukio hilopamoja na kuchangia kupitia 0150000M4WC00 CRDB na 51410029237 zote kwa jina la Kasulu Cathedral Choir pasipo kujali tofauti zao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news