DAR-Klabu ya Simba Sc imethibitisha kuwa mchezo wake wa mkondo wa pili wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane utakaopigwa tarehe 25 Mei 2025 utafanyika katika uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar kama ilivyoamriwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mei 19, 2025 na Afisa Mtendaji Mkuu klabu hiyo, Zubeda Sakuru imeeleza kuwa licha ya jitihada zote zilizofanywa na Serikali, TFF na Klabu katika kuhakikisha mchezo huo unafanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa imeshindikana huku ikiwaomba mashabiki na wapenzi wetu kuwa watulivu katika kipindi hiki.
“Aidha, tutatoa taarifa rasmi za mchezo huu na hatma ya mashabiki wetu kuelekea katika mchezo huu muhimu kupitia Mkutano Maalumu na wanahabari kesho tarehe 20 Mei, 2025 saa 05:00 asubuhi katika Ofisi za Klabu ya Simba, Oysterbay jijini Dar es Salaam;
