DAR-Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana tarehe 8 Mei 2025 jijini Dar es Salaam kusikiliza mashauri yaliyowasilishwa mbele yake.
1.SHAURI LA MAADILI NA. 8/2025 TFF VS THABIT ZAKARIA
Thabiti Zakaria, Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano klabu ya Azam alishtakiwa na Sekretarieti ya TFF kwa kosa la kuchochea umma kinyume na Kanuni ya 73(4) ya Kanuni ya Maadili ya TFF toleo la mwaka 2021.
Kamati ilisikiliza pande zote na kupitia nyaraka na vielelezo vilivyowasilishwa mbele yake. Kamati ilibaini kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kumtia mlalamikiwa hatiani kwa kosa la aliloshatikiwa nalo na imemuachia huru.
