DAR-Lebo ya Muziki ya Kondegang chini ya Harmonize Entertainment Limited ambayo ilikuwa ikisimamia kazi za muziki za msanii Ibraah katika kipindi chote cha mkataba wake, imetoa onyo kali kwa msanii wake huyo kufuatia kauli zake, na matamshi yake anayoendelea kuyatoa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii.
Konde Gang imesema Ibraah bado ni msanii halali wa lebo hiyo na afuate taratibu husika zilizoelekezwa kwenye mkataba wake lasivyo atachukuliwa sheria kali.

