Lionel Messi huyu!

NA LWAGA MWAMBANDE

UKWELI ni kwamba, kwa sasa katika ulimwengu wa soka yupo Lionel Messi mmoja tu. 
Mzaliwa huyo wa Jiji la Rosario nchini Argentina ambapo kwa sasa ana umri wa miaka 37 huku akikipiga katika klabu ya Inter Miami CF amejijengea heshima ambayo si rahisi kufikiwa na mchezaji yoyote akiwa ndani na nje ya dimba.

Hakika,Lionel Messi ni mtu wa kipekee na sifa zake zimejidhihirisha kila anapokuwa. Mosi, amejijengea heshima ya unyenyekevu na nidhamu ya hali ya juu.

Machapisho mbalimbali yanabainisha kuwa, Lionel Messi ni maarufu kwa kuwa na tabia ya utulivu na kutokupenda makuu,hii ni tofauti na wachezaji wengi nyota duniani.

Anaelezwa kuwa,hata akiwa katika kilele cha mafanikio, hujitenga na maisha ya kistarabu na hubakia kuwa mnyenyekevu daima.

Pia, inaelezwa kuwa,ufanisi mkubwa wa Lionel Messi umetokana na bidii ya kazi, siyo tu kipaji, kwani huwa anafanya mazoezi kwa bidii na ni mfuatiliaji wa maendeleo yake binafsi.

Lionel Messi ambaye mara nyingi huonekana akiwa kimya, mwenye tabasamu la aibu, na si mtu wa matukio ya hadhara sana amekuwa mstari wa mbele kugusa maisha ya wengine kwa kadri anavyoweza bila kujali hali yao.

Mshairi wa kisasa, Lwaga Mwambande licha ya kuguswa na maisha ya Lionel Messi, pia ameonesha shauku ya kuona wachezaji wengine ikiwemo kutoka Tanzania wakiiga tabia za namna hii ikiwemo bidii, nidhamu, unyenyekevu, upendo na mshikamano ili vipaji vyao viwe na matokeo bora. Endelea;

¹Kama kweli yuko hivi, mwacheni awe alipo,
Kama anasemwa hivi, habahatishi alipo,
Wasemao si walevi, wapinzani wake wapo,
Lionel Messi huyu, nadhani mnyenyekevu.

²Kama yupo uwanjani, upole wa kwake upo,
Makwanja mengi dimbani, yeye na mpira yupo,
Anaonekana duni, madaruga yakiwepo,
Lionel Messi huyu, nadhani mnyenyekevu.

³Gareth Bale asema, shida ilipokuwepo,
Misuli yake kugoma, usumbufu ukawepo,
Liona kama kakwama, hamu kucheza haipo,
Lionel Messi huyu, nadhani mnyenyekevu.

⁴Hapo
yuko Madrid, upinzani wao upo,
Barcelona Messi hodi, ndipo alipokuwapo,
Simu kutosha idadi, kwa Gareth ikawepo,
Lionel Messi huyu, nadhani mnyenyekevu.

⁵Misuli kumsumbua, akataka kusiwepo,
Messi huyu kamwibua, dokta wake alipo,
Shida lipomsumbua, msaada likuwepo,
Lionel Messi huyu, nadhani mnyenyekevu.

⁶Akamshauri Bale, akapate tiba hapo,
Gareth kaenda mbele, tiba njema ikawepo,
Karudi kucheza mbele, afya njema ikiwepo,
Lionel Messi huyu, nadhani mnyenyekevu.

⁷Kujua ni mpinzani, na kuugua kuwepo,
Mwingine ngekula pini, shidi izidi kuwepo,
Ili kule uwanjani, ushindani usiwepo,
Lionel Messi huyu, nadhani mnyenyekevu.

⁸Mesi japo mchezaji, utu wake ukawepo,
Kumuona mshikaji, kwamba kwake shida ipo,
Kafanya wake mtaji, usaidizi uwepo,
Lionel Messi huyu, nadhani mnyenyekevu.

⁹Maarufu
sana huyu, mfano wake haupo,
Ameshinda sana huyu, kumbukumbu zake zipo,
Ila mtu sana huyu, mifano ya kwake ipo,
Lionel Messi huyu, nadhani mnyenyekevu.

¹⁰Wengi
watu maarufu, nyodonyodo zao zipo,
Wengine kwao wachafu, na msaada haupo,
Lionel twamsifu, kwamba bado utu upo,
Lionel Messi huyu, nadhani mnyenyekevu.

Lwaga Mwambande (KiMPAB
lwagha@gmail.com 0767223602

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news