BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha shilingi 291,533,139,000 kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu na vipaumbele vya wizara hiyo, kwenye Mkutano wa 19 wa Bunge uliofanyika mjini Dodoma Mei 16, 2025.

Katika fedha hizo, shilingi 14,485,656,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na kati ya hizo, shilingi 6,958,609,000 ni kwa ajili ya mishahara (PE) na shilingi 7,527,047,000 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo.
Aidha, wizara inakadiriwa kutumia shilingi 277,047,438,000 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo kati ya fedha hizo, shilingi 98,480,905,000 ni fedha za ndani na shilingi 178,566,578,00 ni fedha za nje.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo














