Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, ameondoka nchini Mei 17, 2025 kuelekea Brasilia, Brazili, kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Pili wa Brazili na Afrika kuhusu usalama wa chakula, mapambano dhidi ya njaa na maendeleo vijijini.
Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kuanzia Mei 20 hadi 23, 2025, utawakutanisha wakuu wa nchi na wa serikali, mawaziri wa kilimo kutoka Afrika, mashirika ya kimataifa, Benki ya Dunia pamoja na wataalamu mbalimbali kutoka duniani kote.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo















