ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi leo amemuapisha,Bw.Kombo Hassan Juma kuwa Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Baraza la Mapinduzi, Ikulu leo tarehe 15 Mei 2025.


