ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewaongoza maelfu ya mashabiki wa soka hapa nchini waliojitokeza kushuhudia Mchezo wa Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Mechi hiyo baina ya Simba SC na RS Berkane imechezwa katika Uwanja wa New Amaan Complex, ambapo kwa mara nyingine tena, Simba imeshindwa kutwaa kombe hilo baada ya kutoka sare ya bao 1–1.Kwa matokeo hayo jumla ya magoli matatu kwa moja, RS Berkane kutoka Morocco imetawazwa kuwa Bingwa wa Kombe la Shirikisho kwa msimu wa 2024/2025.
Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amekabidhi kombe hilo kwa Nahodha wa RS Berkane, Issoufou Dayo.

















