Rais Dkt.Mwinyi mgeni rasmi kilele cha Kongamano la eLearning Africa

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Mei 9,2025 anatarajiwa kufunga rasmi Kongamano la 18 la Kimataifa na Maonesho kuhusu Elimu ya Kidijitali, Mafunzo na Ukuzaji wa Ujuzi (eLearning Africa).
Kongamano hilo ambalo lilianza Mei 7,2025 limefunguliwa Mei 8,2025 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es likiwa ni la pili kufanyika hapa nchini tangu liasisiwe mwaka 2005.

Likiwa na dhamira ya kuimarisha elimu ya kisasa, kongamano hilo ambalo limefanyika kwa siku tatu limewakutanisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Pia, awali mawaziri kutoka nchi 19 barani Afrika walishiriki kikao maalumu (Ministerial Roundtable).

Dhamira ikiwa ni kujadili mikakati mbalimbali ikiwemo kuandaa rasilimali watu yenye maarifa na ujuzi pamoja na kuhamasisha matumizi ya teknolojia za kidijitali katika sekta mbalimbali hususani elimu barani Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news