DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan amemteua Abdul-Razak Badru kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA).
Kabla ya uteuzi huu, Badru alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ambapo anachukua nafasi ya Dkt. Elirehema Joshua Doriye ambaye uteuzi wake umetenguliwa.Vilevile,Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Dkt. Rhimo Nyansaho kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ambapo kabla ya uteuzi huu, Dkt. Nyansaho alikuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Azania.
Dkt. Nyasaho anachukua nafasi ya Abdul-Razak Badru ambaye ameteuliwa kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA).
